Click Here to Chat
Hi, What's on your mind?

Lugha ya Kiswahili

By Outworkerpost Support  2 years, 2 months ago

SwahiliPhoto: Swahili

Historia ya Kiswahili

Katika ulimwengu wa mazungumuzo na taaluma kumekuwa na mitazamo mitatu kuhusu fasili ya lugha ya Kiswahili. Katika mtazamo wa kwanza, ingawa si kwa umuhimu, Kiswahili kimefasiliwa kuwa lugha ya kiarabu; katika mtazamo wa pili lugha hii imefasiliwa kuwa lugha chotara iliotokana na mchanganyiko wa ama lugha za kibantu au lugha nyingine za pwani na kiarabu; katika mtazamo wa tatu Kiswahili kimefasiliwa kuwa mojawapo ya lugha za kibantu. Kwa kuwa mitazamo hii imeleta mijadala na utatanishi mwingi ni vyema kuwa makini unapo ulizwa swali kuhusu historia ya Kiswahili kizingatia mitazamo yote tatu.

Maana ya lugha

Lugha ni mfumo wa sauti nasibu zenye kubeba maana na ambazo zimekubaliwa na jamii ya watu Fulani zitumike katika mawasiliano. Kwa hivyo, lugha ni chombo muhimu kinachotumiwa kwa mawasilian.

Dhima ya lugha

Lugha ina jukumu la kutekeleza katika maisha yetu ya kila siku. Tunatumia lugha kwa njia moja au nyingine. Bila lugha mawasiliano yangekuwa balaa. Maisha ya binadamu yangekuwa yamejaa migogoro, migongano, kutoelewana, mafarakano na mengine mengi yasiyokuwa na faida. Ni kwa kupitia lugha watu wanapoweza kuwasiliana.

Irabu, Konsonantina herufi mwanbatano

Alfabeti ya Kiswahili

Alfabeti ya Kiswahili ina herufi zifuatazo

A             b             ch           d             dh           e             f              g             gh           h             I              j              k               l              m            n             ng’         ny           o             p             r              s             sh           t              th               u             v             w            y             z

Kati ya herufi hizi kuna irabu na konsonanti

Tofauti kati ya irabu na Konsonanti ni kwamba irabu hutamkwa kwa ulaini ilhali konsonanti inapotumkwa sauti hubanwa pahali Fulani katika mkondo wa sauti.

Irabu

Irabu pia huitwa vokali.

Katika lugha ya Kiswahili kuna irabu tano.

a             e             i              o             u

Konsonanti

Zifuatazo ndizo Konsonanti za Kiswahili

B             ch           d             dh           f              g             gh           h             j              k             l              m            n               ng’         ny’          p             r              s             sh           t              th           v             w            y             z

 

 

Vitendawili

Kitendawili ni kauli fupi na huwa ni aina ya fumbo. Fumbo hili hutolewa kwa njia inayofanana na swali. Huwa kuna pande mbili- swali na jibu yaani,, fumbo na ufumbuzi.

Mifano ya vitandawili

1.      Afahamu kuchora lakini hajui achoracho. (jibu ni Konokono)

2.      Ajenga ingawa hana mikono (jibu ni ndege)

3.      Ajifungua na kujifunika (jibu ni mwavuli)

4.      Akitokea watu hudhoofika (jibu ni ugonjwa)

5.      Aliwa, yuala, ala, aliwa (jibu ni papa)

6.      Amefunika kote kwa blanketi jeusi (jibu ni giza)

7.      Anakuangalia tu wala hakuoni (jibu ni picha)

Fumbo au mafumbo

Fumbo ni chemshabongo yenye utata inayohitaji kutatuliwa kwa kufikiri kwa makini

Kwa mfano

Mama mmoja aliondoka kwenda shambani huku amembeba motto mchanga. Alipowasili shambani, alimlaza mwanawe kwenye kivuli cha mti na akaanza kulima.  Mara akatokea nyani aliekuwa mtini akamchukua Yule mtoto na kukwea naye mtini. Mama huyo atafanya nini ili ampate mwanawe salama.

Jibu

Ataweka ndizi pahali aliokuwa ameweka mtoto. Naye nyani akiona ndizi atamrudishia mtoto na kuchukua ndizi.